Genesis 22:11-15

11 aLakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Ibrahimu! Ibrahimu!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

12 bAkamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

13 cIbrahimu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 dIbrahimu akapaita mahali pale Yehova-Yire.
Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa.
Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

15 fBasi malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu kutoka mbinguni mara ya pili,
Copyright information for SwhKC